Alhamisi, 4 Juni 2015

BVR Kujiandikisha kwa BVR, Kajiandikishe - Ni siku 7 kwa kituo. Usikose

Mbali na kitambulisho hichi kutumika kupigia kura, pia kitakutambulisha wewe. Ni nyaraka muhimu kuwa nayo. Usikose.


Mchungaji na uongozi wa Kanisa kwa ujumla, tunakutia moyo ukajiandikishe

Mwongozo ni huu hapa kuwa:

Info Po
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI 

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA 

MIKOA YA ARUSHA, KILIMANJARO, MARA NA MANYARA.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mikoa mine (4) ya Arusha, Kilimanjaro, Mara na Manyara kuwa itaendesha zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia ya Biometric Voters Registration'.

Zoezi hilo la Uboreshaji litanzia tarehe 09/06/2015 hadi 09/07/2015.

Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vitongoji, Mitaa na Vijiji katika Kata zote za Mikoa hiyo mine iliyotajwa. Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-. 
  • Waliotimiza umri wa Miaka 18 na watakaotimiza Miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba 2015. 
  • Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura iii kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura. 
  • Wote ambao wanazo sifa lakini hawajawahi kujiandikisha 
  • Wananchi wanatakiwa kwenda kujiandikisha kwenye vituo vya kujiandikisha vilivyoko ndani ya Kata zao. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwasisitiza wananchi wote katika Mikoa hiyo minne kujitokeza kwa wingi ill waweze kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwani ndiyo hatua muhimu ya kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu na kuchagua viongozi wao. Uandikishaji utafanyika kwa muda wa siku saba (7) kwa kila kituo. 

JITOKEZE SASA NENDA KAJIANDIKISHE 

Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
+255 772 55 55 53
S.L.P. 10923, Dar es Salaam


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni