Alhamisi, 4 Juni 2015

Matangazo ya wiki June 1 - 7, 2015

1. Mzee wa wiki: Mama Magreth Mneney na Shemasi ni Mama Frida George na Elizabeth Petro

2. Wazee wote wa kanda mnapaswa kuandaa na kuwasilisha taarifa za kanda zenu kwa mzee wa kanda kiongozi ifikapo June 3, 2015 hapa kanisani saa 10 jioni

3. Chama cha wanaume na WWK mnakumbushwa kukutana kama ratiba zenu zilivyo

4. Kama mlivyoombwa wazazi kuchanga Tsh 5,000, tafadhali mnaombwa mtakaleze kwani June 1 - 7, 2015 ndio wiki ya watoto

5. Kutokana na ile shule ya watoto yatima inayojengwa na kanisa letu la TAG kule Kabuku - Tanga, kila mzazi unaombwa kuchanga Tsh 4,000 ikapo mwisho wa mwaka huu. Idara ya watoto mnatiwa moyo kulisimamia jambo hili kwa ufanisi

6. Kanisa letu la mahali pamoja GCC linaendelea kufundisha misingi 16 ya imani yetu kwenye ibada za cell, tafadhali jitahidi kushiriki ibada za cell

7. Mpango wetu wa kila mshirika kumshuhudia mtu mmoja kwa mwaka huu, unaendelea na kila mtu timiza makubaliano yetu

8. Tunawashukuru nyote mliojitahidi kumaliza ahadi zenu kuhusu kontena tunalolitarajia kutoka Hong Kong, tafadhali kama bado, unatiwa moyo kujitahidi


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni