Jumanne, 28 Aprili 2015

Unapata somo gani kwa gari hili kuangukiwa na daraja?

Siku zote daraja hili lipo
Magari huwa yanapita
Daraja lilikuwa la kuanguka lakini kwanini litegee wakati gari limefika?
Watu saba walikwepo ndani ya gari hili na wote wamefariki.
Somo ni lipi tunalipata hapa?
Fungua mahali imeandikwa 'Tunalindwa kwa nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata......'
Weka mstari huo sehemu ya maoni hapa chini

Biblia za Mzee Kyejo --- Unakumbuka?

April 19, 2015
Zile Biblia tano za kiswahili alizozitoa Mzee Kyejo, ziliwekwa wakfu na kugawiwa kama ilivyopangwa na hata hivyo Mkurugenzi wa Compassion naye alituongezea Biblia 2 za Kingereza kwani kulikuwa na uhitaji
Biblia ndio hizo hapo mezani na Mchungaji anatafakari namna ya kuziweka wakfu ili zikamjenge atakayepokea

Mchungaji Mwandamizi ajitolea Mwl wa mziki kuja kufundisha hapa GCC

Hizi ni baadhi ya picha
Darasa lilikuwa April 27, 2015 saa 1 jioni mpaka saa 8 usiku
na
Lingine litakuwa April 30, 2015 saa 5 asbh mpaka saa 12 jioni

Wote wenye moyo mnaalikwa, karibuni



Zawadi ya Tsh 500 toka kwa katibu kwa atakayebunia na kuweka jibu hapa chini

Tazama kwa makini picha hii kisha jibu swali hapo chini
Hapa ni wapi alipo huyu kijana? Mtu wa kwanza kujibu na kuweka maoni yake chini kwenye nafasi ya maoni basi atakuwa amejinyakulia Tsh 500 hela halali kwa malipo ya kiasi hicho. Utatangazwa mshindi hapa hapa kwenye blog yetu

Hawavumi ila wapo tu wametulia - Eze atuzwa hela kwa step alizocheza

Aisee huwezi amini, hata wale wanaoshinda kwenye mazoezi wangetolewa jasho na step alizocheza Eze wakati Mkurugenzi na Hakimu akiimba.
Anayejua Eze alituzwa Tshs ngapi atujuze


Ujumbe WWK - Bodi ya Taifa ulipotembelea GCC

Wageni wakitambulishwa na Mwenyeji wao, ambaye ni Mchungaji wetu

Mhudumu wa leo, Mama mkongwe kwenye huduma

WWK-GCC wakiwatunuku zawadi wageni hawa

Wageni wakishukuru

Unajua 'Endomononi' ni nini?

Hizi ni familia mbili tofauti
1. Mrs Adelaide Kilovera alivyotaka uzazi wa Promise Kilovera, na
2. Mrs Juliana Gidamon alivyotoka uzazi wa David J. Gidamon

Asante Bwana Yesu kwa uzao. Walinde watoto hawa tunakuomba.
Kwa Jina la Yesu, aamen

WWK wakafanya uchaguzi April 26

Hizi ni picha kuanzia Uongozi wa awali kujiuzulu mpaka huu mpya kuchaguliwa.
Mama Neema Kiroya amechaguliwa ila hayuko pichani
Uongozi wa zamani ukajiuzulu

Wasimamizi wa kuraWazee wa kanisa wakifanya kazi yao

Wazee Wa Kanisa wakihesabu kura

Uongozi ukatambulishwa ila Mrs Kiroya hakwepo

Mrs Anney akachaguliwa kuwa Mwenyekiti,
Mrs Kiroya akawa Makamu,
Mrs Mawanja akawa Katibu,
Mrs Justine akawa Naibu Katibu,
Mrs Jonathan akawa Mhazini na
Mrs Kilonzo akawa Naibu Mhazini

Jumatano, 22 Aprili 2015

Familia ya Mchungaji Kiongozi ikatoa Shukrani April 19, 2015

Ni Picha tu tunaweka hapa, maneno tuliyasikia sote pale GCC.

Psalms 7:17 Nitamshukuru Bwana kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu.

Psalms 9:1 Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;

Psalms 18:49 Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.

Psalms 28:7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.

Psalms 30:12 Ili utukufu wangu ukusifu, Wala usinyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, Nitakushukuru milele.

Psalms 35:18 Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi.




Dogo akitoa neno la Shukrani kwa Bwana Yesu

Jumamosi, 18 Aprili 2015

Nia ya kubadili aina ya viti tunavyotumia hapa GCC iko palepale - Tunasonga mbele

Unakumbuka ilianzaje? Ona picha hizi hapa chini siku Mchungaji Kiongozi akizindua kampeni hii

Viti vitatu kwanza na leo tuna viti 21
Kila Kanda imepangiwa idadi ya viti, mfano....
Sinoni viti 40
Sinoni Ngarash viti 19
TMA viti 40,
Bomani viti 30
Olarash viti 20
Mjini kati viti 30
Sekondari viti 20
CDTI viti 5 na
Chuo cha Ualimu viti 5