Jumatano, 27 Mei 2015

Toa taarifa ya uendeshaji mbovu wa vyombo vya moto

Info Post
5/28/2015 08:33:00 AM


Kutokana na wimbi la ajali za barabarani linalosababisha vifo vya mamia ya watu na maelfu kujeruhiwa, wananchi wametakiwa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pindi wanapoona kanuni na sheria za barabarani zinakiukwa na madereva wazembe.

Namba iliyotajwa ni 0800 75 75 75 ambayo itapeleka ujumbe utakaofikishwa katika Makao Makuu ya Polisi kisha mawasiliano kufanywa na askari waliopo katika kituo kinachofuata katika barabara linakopita basi hilo ili lisimamishwe. Taarifa za kukamatwa kwa basi husika zitatangazwa moja kwa moja na Radio One na kuoneshwa ITV.

Dondoo ya Afya - Usiweke chakula cha moto kwenye plastic (sharti gumu kwa sasa)

‘Acheni kuweka vyakula vya moto kwenye plastiki ili Msipate Magonjwa’


SERIKALI imewataka Watanzania kuacha kuweka vyakula vya moto katika mifuko ya plasiti kutokana na uwepo wa uwezekano wa kupata magonjwa mbalimbali.
 
Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Stephen Masele wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mkiwa Adam Kimwanga (CUF).
 
Katika swali lake Kimwanga alitaka  kauli ya Serikali kuhusu madhara ya uwekaji wa chakula cha moto katika mifuko ya plastiki na kauli Serikali kuhusu uchafuzi wa mazingira kutokana na kuzagaa kwa mifuko hiyo.

Masele alisema kuweka chakula cha moto katika mifuko ya plastiki kunakuwepo uwezekano wa kemikali zilizotumika kutengeneza mifuko hiyo kuingia kwenye chakula na kukifanya kuwa sumu.

“Sumu hii yaweza kusababisha saratani, kuharibu ukuaji wa mfumo wa uzazi hususan kwa watoto ambao bado kuzaliwa, mabadiliko ya kijenetiki, matatizo ya kuona, uyeyushaji wa chakula tumboni kuwa taabu au kutokamilika na ini kushindwa kufanya kazi,” alisema.
 
Alisema madhara mengine ni pamoja na kuharibika kwa mfumo wa utendaji wa figo na magonjwa yanayohusiana na mfumo wa kupumulia.
 
“Ninawashauri wananchi wasitumie mifuko ya plastiki na vifungushio vyake kuwekea na kuhifadhia chakula kutokana na madhara yanayoweza kutokea,” alisema.
 
Aliwataka badala ya kutumia mifuko hiyo watumie vifungashio vya glasi, chuma isiyoshika kutu na vyombo vingine vya asili.
 
Alisema pia Serikali inatambua uchafuzi wa mazingira unaotokana na mifuko ya plastiki na inachukua hatua mbalimbali ikiwemo kupiga marufuku matumizi ya mifuko laini yenye unene wa chini ya maikroni 30 na kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala.
 
Alisema pia Serikali inafanya ukaguzi kwa makampuni, maduka na viwanda vinavyozalisha na kusambaza mifuko ya plastiki nchini ili kujiridhisha kama vinazingatia sheria
via Mpekuzi

Jumatatu, 25 Mei 2015

Dada Katarina akaja na Mumewe na Naropil mtoto wao kumshukuru Mungu hapa GCC



Kwa Kozi zote za Kompyuta hapa GCC, piga 0757388959





Uongozi wa WWK - Jimbo ukafanya maombi hapa GCC

Jikumbushie picha hizi







Kama una nia kugombea Uongozi 2015 Oktoba - RATIBA



Picha mbalimbali Baraza la Waangalizi lilipokutana GCC

























Matangazo ya wiki ya May 24-31, 2015

1. Mzee wa Zamu ni Mzee Lukas Kivuyo
Mashemas ni Ana Mnyau na J. Gidamon

2. Trh 1-7/6/2015 ni wiki yetu watoto, mzazi tunakuomba utuchangie Tsh 5,000. Asante

3. Kuna shule ya watoto yatima inajengwa na kanisa la TAG kule Kabuku - Tanga, kila mzazi amwezeshe mwanawe kuchanga Tshs 4,000 kwa mwaka huu

4. Ifikapo August 2015, watu wote wanaoishi pamoja kama mke na mume na wote au mmoja wao ni mshirika wetu, sharti wawe wamesajili ndoa yao kuendana na matakwa ya sheria na taratibu za nchi

5. Endelea kujiandaa kwa ajili ya wiki ya Pentekoste, utatangaziwa utaratibu

6. Kanisa letu limeanza utaratibu wa kufundisha misingi 16 ya Imani yetu kwenye CELL, kila mmoja wetu anaombwa kuwepo kwenye ibada za cell kwani ushirika wako utathibitika kama unaijua na unaishi kwa hiyo misingi. Waalimu wote wachukue masomo ama wasome kwenye blog yetu. Pia kila mshirika anatiwa moyo kuwa na nakala yake

7. Familia ya Ima Kilimbei imebarikiwa kumpata mtoto, mama na mtoto hawajambo

8. Wanawake wote mnaombwa kukutana hapo nje kwa ajili ya kupeana utaratibu wa ratiba zenu wiki hii

9. Mpango wetu wa kila mshirika kumshuhudia mtu mmoja unaendelea na unatiwa moyo kujitahidi

10. Tunawashukuru nyote mliojitahidi kukamilisha ahadi zenu kuhusu ukomboaji wa Container mara likifika bandarini, mliobado mnatiwa moyo kukamilisha

11. Maandalizi ya semina kubwa ya vijana inaendelea na Uongozi wa Idara unatiwa moyo kuonana na Mchungaji kwa ajili ya ukamilishaji wa maandalizi. Semina ni June 12-14, 2015

12. Pamoja na waliodhaifu, na waliosafiri, Mzee Anney anaomba maombi kwani atasafiri kuelekea DSM





Alhamisi, 14 Mei 2015

Nchi ya Burundi yatikisika - Tuiombee Tanzania

Mnamo 13 mwezi May jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidiz mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.Rais Nkurunziza alidaiwa kurudi nchini Burundi kutoka Tanzania ,lakini imethibitishwa kuwa leo, alishindwa kufanya hivyo na kwamba yungali nchini Tanzania.
18.05pm-Wanajeshi watiifu
Wanajeshi watiifu wapiga doria Bujumbura
Makundi hasimu ya jeshi la Burundi yamekuwa yakipambana kukidhibiti chombo cha kitaifa cha habari RTBN ambacho kilizimwa kwa mda .Duru zimearifu kuwa kituo hicho cha habari kiko chini ya udhibiti wa vikosi vinavyomtii rais Pierre Nkurunziza.
17.53pm-Viongozi wajadili Burundi
Baraza la usalama la umoja wa Afrika laijadili Burundi kwa sasa
Baraza la usalama la umoja wa Afrika limetuma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter likisema kuwa wanachama wa baraza hilo kwa sasa wanaijadili.
17.00pm-Wanajeshi wapiga doria
Maafisa wa polisi wapiga doria Burundi
Maafisa wa polisi waliojihami katika mji mkuu wa Burundi,Bujumbura wanaonekana wakilinda vizuizi vya barabarani leo
16.50pm-Mkutano kuhusu Burundi waendelea.
Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Afrika
Baraza la usalama la umoja wa Afrika kwa sasa linaijadili Burundi.
tweets: "Chini ya Uongozi wa balozi Amina Diallo wa Niger,ni mkutano wa 507.Baraza hilo linaangazia hali ilivyo Burundi
16.10pm-RNTB yarudisha matangazo
Kituo cha redio
Kituo cha redio cha Burundi RNTB kimerudi hewani,chini ya wanajeshi walio watiifu kwa rais Pierre Nkurunziza kulingana na duru kutoka kwa wanajeshi.Tumethibitisha kuwa kimeanza kurusha tena matangazo.
15.50pm-Nkurunziza asema yuko tayari kusamehe
Ris wa Burundi Pierre Nkurunziza
Shirika la habari la Reuters limenukuu baadhi ya mahojiano yaliofanywa na rais Nkurunziza na kituo cha habari cha RTNB mapema leo.
''Ninalishtumu kundi lililopanga mapinduzi'',alinukuliwa akisema.
''Nwashkuru wanajeshi wanaorudisha hali ya kawaida na namsamehe mwanajeshi yoyote ambaye yuko tayari kusalimu amri''.
Lakini baada ya mahojiano hayo kulikuwa na vita karibu na kituo hicho cha habari ambacho kwa sasa kimezimwa.
15.47pm-Ramani ya Burundi
Ramani ya Burundi
Ramani ya taifa la Burundi.
15.45pm-Mji wa Bujumbura
Burundi
Mji wa Burundi Bujumbura ulivyo kwa sasa
15.30pm-Vyombo vya habari vyazimwa
KItuo cha habari cha Isanganiro
Kituo cha habari cha Burundi Isanganiro kimesema kuwa kimefungwa na vituo vyengine vya kibinafsi .Kituo hicho ni miongoni mwa vile vilivyotangaza mapinduzi siku ya jumatano.
15.17pm-Kituo cha habari
Askari Burundi
Kituo cha habari cha Redio ya RTNB kimezimwa kufuatia mapigano makali karibu na afisi zake mjini Bujumbura.
15.01pm:Rais wa Burundi Ahojiwa
Wanajeshi nchini Burundi wakipiga doria
Kituo cha habari cha Burundi RTBN kimemhoji rais Pierre Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita.Vita vimezuka karibu na afisi za kituo hicho cha habari.Jenerali anayeunga mkono jaribio hilo la mapinduzi amekiambia chombo cha habari cha AFP kwamba vitengo vinavyopigana kumpindua vimepata agizo la kukiteka kituo hicho habari cha RTNB kwa kuwa wana uwezo.
14.30pm:Makundi ya vijana waliojihami
Vijana Burundi
Kuna madai kwamba kundi la vijana linalunga mkono serikali limeshambulia kituo kimoja cha habari cha kibinafsi mjini Bujumbura.KUndi hilo linalojulikana kama Imbonerakure,baadhi ya watu wanaamini kwamba vijana hao wanatumiwa kama wapiganaji na kwamba huenda wamepewa silaha ili kuwatishia raia kabla ya uchaguzi.
13.45pm-Hali ni tete Burundi
Wanajeshi wa BUrundi
Hali bado ni tete nchini Burundi siku moja tu baada ya jenerali mmoja wa jeshi kujaribu kutekeleza mapinduzi .Barabara nyingi zimeendelea kuwa bila watu kwa kipindi kirefu cha alfajiri huku wengi wakisalia ndani ya majumba yao wakihofia usalama kulingana na mwanahabari wetu Ruth Nesoba.
13:30pm-Ukabila
Kiongozi wa jeshi aliyetangaza mapinduzi
Tofauti zilizopo katika jeshi la Burundi kufuatia jaribio la mapinduzi hazionekani kuwa katika misingi ya kikabila ,mkuu wa majeshi ambaye ni mtiifu kwa rais Nkurunziza pamoja na jenerali wa majeshi aliyetangaza mapinduzi hayo ni wa kabila la Hutu.Makundi hayo yanaonekana kugawanyika kati ya wale wanaoamini rais Nkurunziza alikiuka makubaliano ya amani yaliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kutaka kuongoza kwa muhula wa tatu na wale wanaosalia kuwa watiifu kwake
12:05pm-Wanajeshi watiifu
Mj wa Burundi Bujumbura
Afisa mmoja wa kijeshi ameiambia BBC Afrique kwamba wanajeshi watiifu nchini Burundi wanadhibiti mji wa Bujumbura ,uwanja wa ndege,makao ya rais pamoja na vituo vya redio na runinga.
12:00pm-Milio ya Risasi
Wanajeshi wa Burundi
Makundi hasimu ya askari yanakabiliana katikati mwa mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.