Jumamosi, 11 Aprili 2015

Matangazo Muhimu wiki inayoishia April 12, 2015


1. Mzee wa Zamu: Mzee Kivuyo

2. Shemasi wa Zamu: Joseph Gidamon na Anna Mnyau

3. Mwaka 2015 ni mwaka wa malango kuwa wazi, kila mshirika anakumbushwa kutimiza wajibu wake ili baraka hizo ziweze kumjia na kumpata

4. Trh 12/4/2015 ni siku ya tamasha kubwa la kumsifu na kumwabudu Mungu wetu hapa kanisani, karibuni nyote. Ni kuanzia saa7 mchana mpak baadaye

5. Ijumaa ni siku ya mkesha maalum na wote tutakuwa tumefunga kwa saa24

6. Ibada zetu wiki hii zitaendelea kama kawaida kwa maana ya kwamba, Jumanne ni siku ya ibada za cell, Jumatano ni mafundisho ya Biblia, Ijumaa ni ibada ya maombi saa 10 jioni na kufuatiwa na mkesha saa 3 usiku na Jumapili ni ibada ambapo kutakuwa na ibada ya kwanza saa1 asubuhi, maandiko saa3:30 asubuhi, ibada ya pili saa4:30 asubuhi na kisha Tamasha la kusifu kuanza saa7 mchana

7. Mzee wetu Kiongozi hayupo kati yetu kwani amefiwa na baba yake mkubwa, pia Mzee Maginga ni mgonjwa na Mzee Kyejo amesafiri kuelekea Dsm - Tuwaombee

8. Serikali ya Tanzania kupitia NEC imesogeza mbele zoezi la kuipigia kura katiba inayopendekezwa lakini bado tarehe 20-25/4/2015 ni wiki ya kuisoma na kuilewa katiba hiyo inayopendekezwa hapa kanisani.

9. Tunawakumbusha nyote mlioahidi kwa ajili ya kukomboa Container, mweze kuanza kutimiza ahadi zenu

10. Kama ambavyo kadi ya mwaliko imetolewa kwa Kanisa zima, Sote tuhudhurie kumwaga binti yetu Grace anayetarajiwa kuolewa April 9, 2015 kule Serengeti. SendOff itafanyika ukumbi ulioko chuo Cha Biblia Ngaramtoni. Karibuni sana

11. Kulingana na mpango mkakati wa kanisa, kila mshirika anakumbushwa kuendelea kutimiza wajibu wake tuliokubaliana kila mmoja wetu kumshuhudia mtu mmoja aokoke, asimame na aendelee mbele

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni