Jumapili, 12 Aprili 2015

Watu wasiokuwa na Biblia GCC

Wahenga wa kule Nadosoito waliwahi kusema 'Mzaha mzaha hutu......'

Mnamo March 15, 2015 Mzee wetu Kyejo alihudumu hapa kanisani na katika kuhudumu kwake, alisema mtu yeyote asiye na Biblia ajiandikishe kwa Katibu wa GCC ili kadri Mungu atakavyombariki, basi anunue Biblia kwa ajili ya watu hao.

Wiki ya kwanza ikapita, hakuna aliyejiandikisha

Wiki ya 2, 3, na mpaka leo hakuna aliyejitokeza

Si kwamba watu wote wana Biblia, siku ile waliambiwa waoneshe Biblia zao, wengi hawakuwa na Biblia

Sasa Biblia zimekuja na Mzee Kyejo ameshauri kuwa basi apewe atakayepewa lakini baadaye akabadili mawazo kuwa Kanisa liweke utaratibu mwingine kutumia Biblia hizo

Ona Mzee akikabidhi Biblia hizo


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni