Jumapili, 12 Aprili 2015

Matangazo ya wiki hii 13-19/4/2015



1. Mzee wa Zamu: Mzee Magreth Mneney

2. Shemasi wa Zamu: Frida George na Elizabeth Petro

3. Mwaka 2015 ni mwaka wa malango kuwa wazi, kila mshirika anakumbushwa kutimiza wajibu wake ili baraka hizo ziweze kumjia na kumpata

4. Leo ndio Trh 12/4/2015, siku ya tamasha kubwa la kumsifu na kumwabudu Mungu wetu hapa kanisani, karibuni nyote. Ni kuanzia saa7 mchana mpak baadaye

5. Ijumaa ni siku ya mkesha maalum na wote tutakuwa tumefunga kwa saa12

6. Ibada zetu wiki hii zitaendelea kama kawaida kwa maana ya kwamba, Jumanne ni siku ya ibada za cell, Jumatano ni mafundisho ya Biblia, Ijumaa ni ibada ya maombi saa 10 jioni na kufuatiwa na mkesha saa 3 usiku na Jumapili ni ibada ambapo kutakuwa na ibada ya kwanza saa1 asubuhi, maandiko saa3:30 asubuhi, ibada ya pili saa4:30 asubuhi na kisha Tamasha la kusifu kuanza saa7 mchana

7. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia NEC imesogeza mbele zoezi la kuipigia kura katiba inayopendekezwa lakini bado tarehe 20-25/4/2015 ni wiki ya kuisoma na kuilewa katiba hiyo inayopendekezwa hapa kanisani.

8. Tunawakumbusha nyote mlioahidi kwa ajili ya kukomboa Container, mweze kuanza kutimiza ahadi zenu

9. Kulingana na mpango mkakati wa kanisa, kila mshirika anakumbushwa kuendelea kutimiza wajibu wake tuliokubaliana kila mmoja wetu kumshuhudia mtu mmoja aokoke, asimame na aendelee mbele. Na leo unagawiwa kijitabu kimoja ukisome, uelewe kisha umshuhudie mtu mmoja na kumpa kijitabu hicho

10. Wanaume wote mnakumbushwa kukutana kesho saa 10 jioni kwa ajili ya chama chenu

11. Jumapili ijayo familia ya Mchungaji itatoa sadaka ya shukrani, tunaombwa tumshukuru Mungu pamoja nao

12. Kuanzia sasa utakuwa ukipata matangazo na habari zote za GCC kupia gccmonduli.blogspot.com


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni