Jumanne, 5 Mei 2015

Maandiko karibu yote yenye kuhusu Zaka/Fungu la kumi - Jifunze

Matendo makuu ya Bwana kwetu iwe hamasa ya kutoa fungu la kumi Mwanzo - 14:20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.

Haipaswi kuacha kutoa fungu la kumi - Kumb 14:22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

Hata ikitokea hukutoa, siku utakayotoa, toa kwa kiasi ulichokuwa hujatoa - Kumb 14:28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;

Vitu vinavyopaswa kutolewa fungu la kumi  ni vya aina nyingi sana - Lawi 27:30 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana.

Kama ikitokea unataka kubadili kitu cha fungu la kumi, unatoa chenye thamani ya kile ambacho ungetoa na kuongeza sehemu ya tano juu yake - Lawi 27:31 Na kama mtu akitaka kukomboa cho chote cha zaka yake, ataongeza sehemu yake ya tano juu yake.

Namna ya kujua fungu la kumi ni kuhesabu vitu na ile ya kumi ndio ya kuitoa - Lawi 27:32 Tena zaka yote ya ng'ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa Bwana.

Kwa nini kutoa fungu la kumi/zaka? - Hesabu 18:21 Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.

Nani watumiaji wa Zaka? Hesabu 18:24 Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote.

Watumiaji nao wana mwongozo wao - Hesabu 18:26 Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka. Pia Hesabu 18:28 Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana.

Kuna pa kupeleka zaka na sadaka. Sio kwa ombaomba - Kumb 12:6 pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng'ombe na ya kondoo; Pia Kumb 12:11 wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua Bwana, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa Bwana. Kumb 12:17 Usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng'ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zo zote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako;

Kupeleka mahali maalum alipopachagua Bwana/Kanisani, ni ishara ya ibada yenye matokeo ya kujifunza kumcha Mungu - Kumb 14:23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.

Ukisha toa Zaka, inakuwa wewe umemaliza sehemu yako - Kumb 26:12 Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;

Vitu vya kutolewa zaka, ni pamoja na plot/shamba --- kwa ujumla ni kila kitu ambacho ukihesabu, inafika kumi - 2 Nyakati 31:5 Mara ilipotangaa amri, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, na divai, na mafuta, na asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta nyingi. Ona pia 2 Nya 31:6 Nao wana wa Israeli na Yuda, waliokaa mijini mwa Yuda, wakaleta pia zaka za ng'ombe na kondoo, na zaka za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyowekewa Bwana, Mungu wao, wakaviweka chungu chungu. Pia Nehemia 10:37 tena tuyalete malimbuko ya unga wetu, na sadaka zetu za kuinuliwa, na matunda ya miti ya namna zote, mvinyo, na mafuta, kwa makuhani, hapo vyumbani kwa nyumba ya Mungu wetu; na zaka za ardhi yetu kwa Walawi; kwa kuwa hao Walawi wazitwaa zaka mijini mwote mwa kulima kwetu.

Hao wenye kupokea zaka, wataweka utaratibu wao wa usimamizi kwa uaminifu wa vitu hivyo - 2 Nyakati 31:12 Wakayaingiza matoleo na zaka na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu; na juu yake Konania Mlawi alikuwa mkuu, na wa pili ni Shimei nduguye.

Zaka hupokelewa na Watumishi wa Bwana. Ndio maana siku hizi hapa GCC, unakaribishwa mbele ili uombewe ishara ya kupokea vitu hivyo - Nehemia 10:38 Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.

Ni wajibu wa watumishi wa Mungu kukufundisha na kukutia moyo kutoa Zaka. Tena inatakiwa uagizwe kutoa zaka - Nehemia 12:44 Na siku hiyo watu wakaagizwa juu ya vyumba vya hazina, kwa sadaka za kuinuliwa, na kwa malimbuko, na kwa zaka, ili kuzikusanya, kwa kadiri ya mashamba ya miji, sehemu zilizoamriwa katika torati za makuhani, na Walawi; kwa maana Yuda waliwafurahia makuhani na Walawi waliotumika.

Hapa GCC panapaswa kuwepo GHALA la kuhifadhia bidhaa mbalimbali za ZAKA ili zitumiwe na watumishi wa Mungu - Nehemia 13:5 alikuwa amemtengenezea chumba kikubwa, hapo walipoweka zamani sadaka za unga, na ubani, na vyombo, na zaka za nafaka, na divai, na mafuta, walivyoamriwa kuwapa Walawi, na waimbaji, na mabawabu; tena sadaka za kuinuliwa zilizokuwa za makuhani. Ona Nehemia 13:12 Ndipo Yuda wote walipoleta zaka za nafaka, na mvinyo, na mafuta, kwenye HAZINA. Na itakuwa ni amri kuleta zaka GHALANI - Malachi 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Ni wajibu kutoa zaka - Amos 4:4 .... kaleteni dhabihu zenu kila asubuhi, na zaka zenu kila siku ya tatu;

Kutokutoa zaka ni kuiba na unamwibia Mungu - Malachi 3:8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.

Zaka hupaswa kuwa kamili kama ambavyo ulivyohesabu - idadi yake toa kamili na itakuwa ni namna ya kumjaribu Bwana - Malachi 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Kutoa zaka hakutoshi pekee kama maisha ya kiroho hayapo sawa, unaelekezwa kutoa zaka huku ukiyapa maisha ya kiroho kipaumbele kikubwa sana - Mathayo 23:23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Na - Luka 11:42 Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili.

Wala sio sifa kutoa fungu la kumi na haitoshi kumpa mtu kibali kwa Mungu. Ni unakuwa tu umefanya yaliyo sehemu yako - Luka 18:12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni