Jumamosi, 2 Mei 2015

Semina ya Ndoa hapa kanisani leo May 2, 2015

Mwl Zakariah toka Chuo Cha Biblia ametushirikisha mengi ila mwisho picha tumeweka hapa

Maisha yataendelea kuwa magumu kama mtu ni mwenyewe.
Ndoa huondoa upweke
Ndoa huleta wajibu
Ndoa huunda familia na kuendeleza uumbaji - Mw 1:28




Mwanzo 4:16 Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni.
 17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe.
 18 Henoko akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; Methushaeli akamzaa Lameki.
 19 Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila.

Kumwacha Mungu ndiko kulikopelekea kuzaliwe uzao wenye kutokujali maelekezo ya Mungu.
Mwalimu ametoa mfano wa kununua vifaa vipya dukani, lazima kuwemo na kijikaratasi cha namna ya kutumia ili uweze kufikia lengo lililokusudiwa. Hata ukiwa unaumwa, kiasi cha dawa ili upone kinajulikana ila ina utaratibu wa kula dawa hiyo ni 2 mara 3 kwa siku kadhaa.
Pamoja na ugonjwa kuweza kuzidi ukiwa unatumia dawa hiyo, huwezi kushauriwa kutumia zote mara moja. Lazima uweke breki
Mijadala ilikuwa mikali lakini kwa wewe uliyekosa basi Boresha ndoa yako

Maoni 2 :

  1. Mshirika wako wa karibu na pekee ni mkeo au mume wako. Baba, mama, ndugu au yeyote hawezi kulinganishwa ama kuchukua nafasi ya mke

    JibuFuta
  2. Kitu kimoja ninachopewa na Mungu ni cha thamani na bora kuliko vitu vingi ninavyoweza kujipa mwenyewe. Hata ningepewa wanawake wote wa mtaa wangu, hawatafikia uzuri, uwema, na uthamani wa mke wangu huyu mmoja niliyepewa na Mungu.
    Hii ni nukuu ya Mwl kwa Martin Luther

    JibuFuta