Jumamosi, 9 Mei 2015

Semina ya viongozi siku ya pili katika picha

Kundi la viongozi wakijadili mambo ya kufanyia maamuzi

Kundi lingine likijadili baadhi ya mambo ya kuamua baada ya semina hii

Mgawanyo wa makundi

Darasa likaanza

Viongozi wakimsikiliza mwalimu

Mwalimu akiwasilisha mada
Mwaswali na maazimio:
1. Kikao kikiitishwa na huji, unakuwa umeamuaje? 
Ni kusema mimi ni mzembe, sijali, sitilii maanani wala haina umuhimu hicho kikao

2. Kutokutafuta walau mrejesho wa kikao, ina maana gani kwako? 
Haina umuhimu kwahiyo sitafuti mrejesho

3. Unadhani udhaifu wa kiongozi wa kiroho unaambatana na ulegevu kiroho? 
Huenda sambamba

4. Kuongoza kulalamika wakati huwajibiki katika nafasi yako ni kusemaje? 
Kiongozi huyu anakuwa na mgomo moyoni na tatizo lake ni sugu

5. Kutoshiriki semina yoyote, ina tafsiri ipi? 
Kujitosheleza yenye ashirio la kupoa kiroho

6. Kama watu hawatoshi kukuelekekeza, nani hatimaye unadhani atafaa kusema nawe?
Ulimwengu siku moja utamfunza kiongozi wa aina hii

7. Ili ukubaliane na jambo, ni kwa njia ipi nzuri uambiwe?
Kwa kuwa kiongozi huyu ana tatizo la kuvamiwa kiroho, ashauriwe na kuombewa

8. Unadhani kuchaguliwa na watu kuwa kiongozi ina muunganiko wowote na kupewa nafasi ya kuongoza na Mungu?
Ndiyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni