Jumamosi, 9 Mei 2015

Uchaguzi wa Uingereza - tuwawezeshe watoto wetu

Uingereza:Mbunge mchanga zaidi miaka 20  8 Mei 2015

Mshirikis
Wapiga kura nchini Scotland wamemchagua mwanafunzi wa chuo kikuu kuwa mbunge wao.
Bi Mhairi Black, alishinda kura za eneo bunge la Paisley and Renfrewshire South na kumbwaga kigogo wa chama cha Labour aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni bwana Douglas Alexander.
Mbali kuzua mjadala kwa kumbwaga kigogo wa chama cha Leba na kumaliza ukiritimba wa chama cha Leba Bi Black sasa ndiye Mwakilishi wa kwanza katika kipindi cha miaka 70 ambaye si mwanachama wa Leba.
Mbunge mchanga zaidi Uingereza Mhairi Black
Aidha ameweka rekodi ya kuwa mbunge mwenye umri mdogo zaidi nchini Uingereza tangu karne ya 17.
Black ana umri wa miaka 20 pekee.
Bi Black anamfuata mbunge mwengine aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo ya 1667, bwana Christopher Moncktook.
Black ana umri wa miaka 20 pekee
Bwana Moncktook alikabidhiwa uongozi akiwa na umri wa miaka 13 .
Wakati huo hata hivyo mamlaka yalinasibishwa na hivyo haikutambuliwa kama uchaguzi haswa.
Bi Black alipotangazwa mshindi akiwa na mpinzani wake Bw Alexander
Lakini Bi Black alihakikisha jina lake linaingia katika kumbukumbu za historia kwa kuvunja rekodi hiyo iliyowekwa miaka 350 iliyopita alipozoa kura 23,548 dhidi ya 17,864 za Alexander.
Majuzi hata hivyo mbunge aliyekuwa akitambuliwa kama mchanga zaidi kuchaguliwa alikuwa ni Charles Kennedy wa chama cha Liberal Democrat aliyechaguliwa akiwa na umri wa mia 23
Hata hawa wanaweza nikiwekeza nguvu zangu kuwajengea ujasiri
Huyu ni jamaa akimpigia mke wangu simu kuwa atarudi saa ngapi

Jamaa mwingine hapa anatest kuwa kwenye mpira kwenye nini hasa

Sasa hapa jamaa anatumia kompyuta kunanii

Sasa ni mipango ya kujitwalia majimbo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni