Jumatatu, 25 Mei 2015

Matangazo ya wiki ya May 24-31, 2015

1. Mzee wa Zamu ni Mzee Lukas Kivuyo
Mashemas ni Ana Mnyau na J. Gidamon

2. Trh 1-7/6/2015 ni wiki yetu watoto, mzazi tunakuomba utuchangie Tsh 5,000. Asante

3. Kuna shule ya watoto yatima inajengwa na kanisa la TAG kule Kabuku - Tanga, kila mzazi amwezeshe mwanawe kuchanga Tshs 4,000 kwa mwaka huu

4. Ifikapo August 2015, watu wote wanaoishi pamoja kama mke na mume na wote au mmoja wao ni mshirika wetu, sharti wawe wamesajili ndoa yao kuendana na matakwa ya sheria na taratibu za nchi

5. Endelea kujiandaa kwa ajili ya wiki ya Pentekoste, utatangaziwa utaratibu

6. Kanisa letu limeanza utaratibu wa kufundisha misingi 16 ya Imani yetu kwenye CELL, kila mmoja wetu anaombwa kuwepo kwenye ibada za cell kwani ushirika wako utathibitika kama unaijua na unaishi kwa hiyo misingi. Waalimu wote wachukue masomo ama wasome kwenye blog yetu. Pia kila mshirika anatiwa moyo kuwa na nakala yake

7. Familia ya Ima Kilimbei imebarikiwa kumpata mtoto, mama na mtoto hawajambo

8. Wanawake wote mnaombwa kukutana hapo nje kwa ajili ya kupeana utaratibu wa ratiba zenu wiki hii

9. Mpango wetu wa kila mshirika kumshuhudia mtu mmoja unaendelea na unatiwa moyo kujitahidi

10. Tunawashukuru nyote mliojitahidi kukamilisha ahadi zenu kuhusu ukomboaji wa Container mara likifika bandarini, mliobado mnatiwa moyo kukamilisha

11. Maandalizi ya semina kubwa ya vijana inaendelea na Uongozi wa Idara unatiwa moyo kuonana na Mchungaji kwa ajili ya ukamilishaji wa maandalizi. Semina ni June 12-14, 2015

12. Pamoja na waliodhaifu, na waliosafiri, Mzee Anney anaomba maombi kwani atasafiri kuelekea DSM





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni