Alhamisi, 7 Mei 2015

Habari mbalimbali kwa ufupi toka humu nchini

Mrema Avuliwa Uanachama TLP


KAMATI ya Ukweli na Maridhiano ya Chama cha Tanzania Labour (TLP), imetangaza kumvua uanachama Mwenyekiti wa chama hicho, Agustino Mrema.
 
Akizungumza jana, jijini Dar es Salaam na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joram Kinanda alisema kuwa kamati hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia kwa kina malalamiko yaliyokuwa yakimuhusu Mrema, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo.
 
Mwenyekiti huyo alisema kuwa mbali na Mrema wengine waliovuliwa uanachama ni Hamisi Mkadamu, Antoni Mapunda, Nancy Mrikaria, Dominata Rwechungura, Maxmilian Lymo, Richad Lyimo, Hamisi Mkumba na Stanley Temba.
 
Kinanda alisema kuwa wanachama hao wamevuliwa uanachama kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, toleo la 2005 Ibara ya 9.9 (c) na 2009 ibara 9.5(c).
 
Kinanda alisema kuwa maazimio hayo yamepelekwa katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa taratibu za kisheria pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
 
Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza, alipotafutwa ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema kamati hiyo haitambuliki kisheria.
 
“Kamati hiyo haitambuliki kisheria, na hata Mrema mwenyewe amekuwa akipinga TLP kuwa na kamati ya aina hiyo na hata viongozi wake hawatambuliki, ” alisema

PICHA: Mvua Yaliharibu Jiji La Dar es Salaam...Polisi Watoa Tahadhari

Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, limetoa tahadhari kwa watumiaji wa barabara kutoka maofisini mapema kufuatia baadhi ya barabara kujaa maji.





Info Post

Ni leo eti, gari lilikuwa linapita barabarani, ghafla mti vuup

Kwingineko...


Hali ya shule baadhi humu nchini
Mtu mmoa amekufa na wengine tisa kujeruhiwa katika maandamano yanayoendelea kupamba moto nchini Burundi kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Mwandishi wa BBC aliyepo mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura anasema mamia ya watu wamejitokea kwenye maandamano hayo huku baadhi wakichoma moto baadhi ya vitu.
Siku ya jumanne Mahakama ya Katiba ilikubali kuwa Rais Nkurunziza anaweza kugombea urais ambapo ilisema ni halali yeye kuwania tena urais kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Katika hotuba yake siku ya jumatano Rais Nkurunziza alisema kama atachaguliwa tena kuongoza nchi hiyo, muhula huu utakuwa wa mwisho kwake kuwa madarakani.

Maoni 1 :