Jumanne, 12 Mei 2015

Tangazo la Nafasi ya Kazi - St. Paul Pre&Pri School

Shule ya St. Paul yenye makao yake katika viwanja vya Glory Christian Centre ina maono ya kutoa elimu bora kwa watoto wote hapa ndani na nje ya mipaka ya Monduli.

Shule basi inamtafuta mwalimu

Masharti:

1. Kibinafsi hata kabla ya barua awe ameokoka
2. Awe na vyeti vinavyotambulika na NECTA
3. Aambatanishe barua ya utambulisho wake iliyotoka kwa mchungaji wa Kanisa la kiPentekoste la mahali pamoja na sio Ministry
4. Katika kanisa hilo la mahali pamoja, awe ni mshirika kwa kipindi kisichopungua miaka miwili na uthibitisho uwepo kuwa akisafiri, huwa anaaga
5. Pamoja na barua ya kuomba nafasi hii, aambatanishe nakala za vyeti vyote husika
6. Wasifu wake (CV) uambatanishwe na uwe maalum kwa ajili ya kazi hii. Yaani, current (Chini yake iwepo sahihi na tarehe kuonesha sasa
7. Picha mkato, yaani, passport size, iwe imebandikwa kwenye barua ya maombi na mhuri wa kanisa tajwa hapo juu ugongwe juu ya picha lakini kwenye barua husika. Isiwe vinginevyo.
8. Kufuta futa na kutosomeka vyema na mwandiko kutokuwa na mvuto huchangia maombi yako kutoshughulikiwa kwani waombaji ni wengi na hivyo muda kutokuwepo wa kujaribu kutafakari unachojaribu kukisema

Tuma maombi yako kuja

Mwenyekiti,
Kamati ya Shule,
St. Paul Pre&Primary School,
S. L. P. 56,
Monduli

Pia waweza kutuma nyaraka hizo kupitia barua pepe hii: egkyejo@yahoo.com

Maombi yako yawe yamekishakupokelewa Juni 15, 2015 lakini kabla ya saa 4:00 asubuhi

Maoni 1 :