Ijumaa, 8 Mei 2015

May 8 saa 10 na May 9, 2015 saa 3asbh - 10jioni SEMINA KUBWA YA VIONGOZI GCC

Mwaliko wa Viongozi wote kuhudhuria semina hii

Waalimu wa Cell,
Katibu wa Cell,
Viongozi wa kamati, Kamati ya Shule, Kamati ya Umisheni, Kamati ya Uinjilisti, Kamati ya ...
Viongozi wa Idara, Idara ya WWK, CMF, CAs, Watoto, Kwaya
Mashemasi,
Wazee wa Kanda,
Wazee wa Kanisa,
Wachungaji

Wote mmealikwa na Mchungaji mhudhurie semina hii.

Uzuri na unyeti wa Semina hii ni kuwa, ikitokea haupo, mwelekeze mke/mume wako akuwakilishe.

Usikose. Usikose. Jitahidi.

Saa 10 jioni leo May 8, 2015 uwe umeshakaa kwenye kiti
Saa 3 asbh May 9, 2015 uwe umeshakaa kwenye kiti

Usikose tena

Kwa mawasiliano, tumia 0768338434

Maoni 1 :

  1. GLORY CHRISTIAN CENTRE
    SEMINA YA VIONGOZI
    MAY 8 – 9, 2015
    Na J. Samson

    Mstari wa kukumbuka: Mdo 8:31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.
    Kila mtu ni kiongozi kwa mwingine.
    Kwanini mtu huyu asimhitaji Mungu amwongoze? Anamhitaji mtu mwenzake amwongoze. Haikanushiki, Kiongozi lazima awepo. Kiongozi huyu ni mimi katika nafasi yangu. Na katika nafasi hii yangu, mimi nami ninamhitaji kiongozi, ndiye huyo au hao walio juu yangu

    Maandiko ya Somo letu leo: Kut 18:13-26

    Kwa mimi kuwa kiongozi, kazi yangu kuu ni kuwaongoza wengine waende mbele - Kut 15:22 Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji (changamoto zenyewe zipo tu).
    Mara ulipochaguliwa kwenye hiyo nafasi yako, kuna mahali unapaswa uwafikishe watu unaowaongoza - Kut 32:34

    Kwa maombi umepatikana, hata kama ulipigiwa kura ama uliteuliwa - Numbers 27: 15. (Umuhimu wa kiongozi unabainika hapa - usijidharau)

    Pamoja na baadhi ya vigezo, watu huchaguliwa kuwa viongozi wa wengine - 1 Nya 15: 19-24

    Kuwa na kiongozi ni mbinu nyingine muhimu ya kusonga mbele - 1 Nya 19:16

    Njia kutonyooka wakati wote, kiongozi lazima kujipa moyo ni muhimu sana ili kufikia malengo - 2 Nya 25:11

    Je, kuna siku umewahi kujitambua kuwa wewe ni kiongozi wa ngazi hiyo uliyoko? Ayu 31:18 Nami nimekuwa ni kiongozi cha mjane tangu tumbo la mamangu

    Kiongozi anapoharibika, waongozwao huonewa na chochote - Isa 3:12. Na ikifikia hatua ya kiongozi kuwakosesha watu wa Mungu, Mungu kuanza kulalamika - Isa 9:16

    Waongozwao nao hugundua ubaya wa kiongozi wao - Omb 3:2 Ameniongoza na kuniendesha katika giza Wala si katika nuru. Mungu huweka tangazo - Micah 7:5 Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini

    Kiongozi kutopata maelekezo toka kwa Mungu kupitia Neno na Maombi, hushindwa kupambanua - Mat 23:16. Pia Mat 23:24

    Kuna utofauti mkubwa sana wa kuongoza kidunia na kuongoza kiroho - Marko 10: 42-45

    Tunakuwa viongozi wazuri kwa sisi wenyewe kuongozwa kwanza na Roho Mtakatifu - John 16:13. Pia tunapewa karama za maongozi - 1Corinthians 12:28
    Kiongozi mzuri huwa mfano kwa kumheshimu kiongozi wa juu yake - Hebrews 13:7 . Hebrews 13:17 . Hebrews 13:24

    Kuna faida nyingi kwa kuwa kiongozi bora - Daniel 12:3

    Ili ufanikiwe kwenye uongozi wako, lazima ushauriane na viongozi wenzako. Usiache kuitisha vikao - 1 Nya 13:1 Kisha Daudi akafanya shauri na maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, naam, na kila kiongozi.

    Jihoji: Kikao kikiitishwa na huji, unakuwa umeamuaje? Kutokutafuta walau mrejesho wa kikao, ina maana gani kwako? Unadhani udhaifu wa kiongozi wa kiroho unaambatana na ulegevu kiroho? Kuongoza kulalamika wakati huwajibiki katika nafasi yako ni kusemaje? Kutoshiriki semina yoyote, ina tafsiri ipi? Kama watu hawatoshi kukuelekekeza, nani hatimaye unadhani atafaa kusema nawe? Ili ukubaliane na jambo, ni kwa njia ipi nzuri uambiwe? Unadhani kuchaguliwa na watu kuwa kiongozi ina muunganiko wowote na kupewa nafasi ya kuongoza na Mungu?

    Kwa leo tunaishia hapa na Mungu awabariki kwa kujitambua kuwa mu viongozi na mkakubali kuanzia sasa kuwa viongozi bora

    JibuFuta