GLORY CHRISTIAN CENTRE
SEMINA YA VIONGOZI
MAY 8 – 9, 2015
Na J. Samson
Mstari wa kukumbuka: Mdo 8:31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.
Kwanini mtu huyu asimhitaji
Mungu amwongoze? Anamhitaji mtu mwenzake amwongoze. Haikanushiki, Kiongozi
lazima awepo. Kiongozi huyu ni mimi katika nafasi yangu. Na katika nafasi hii
yangu, mimi nami ninamhitaji kiongozi, ndiye huyo au hao walio juu yangu
Maandiko ya Somo letu leo:
Kut 18 13 Asubuhi yake Musa akaketi ili awapishie hukumu watu; na hao watu
wakasimama kumzunguka Musa tangu asubuhi hata jioni.
14 Mkwewe Musa alipoyaona yote
aliyowafanyia watu, akasema, Ni jambo gani hili uwatendealo hao watu? Kwani
wewe kuketi hapo peke yako, na watu wote kusimama kwako tangu asubuhi hata
jioni?
15 Musa akamwambia mkwewe, Ni kwa
sababu watu hunijilia mimi wapate kumwuliza Mungu; 16 wakiwa
na neno, hunijilia; nami naamua kati ya mtu na mwenziwe, nami nawajuvisha amri
za Mungu, na sheria zake. 17 Mkwewe Musa akamwambia, Jambo hili ufanyalo si jema. 18 Huna budi utadhoofika wewe, na hawa
watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi
wewe kulitenda peke yako.
19 Sikiza sasa neno langu, nitakupa
shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe
umletee Mungu maneno yao;
20 nawe utawafundisha zile amri na
sheria, nawe utawaonyesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo
inawapasa kuifanya.
21 Zaidi ya hayo utajipatia katika
watu hawa watu walio na uwezo, wenye
kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu
yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa
kumi; 22 nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa
watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe
mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe.
23 Kwamba utafanya jambo hili, na
Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao
watakwenda mahali pao kwa amani.
24 Basi Musa akasikiza neno la
mkwewe, akayafanya yote aliyokuwa amemwambia.
25 Musa akawachagua watu wenye
uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu,
na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi. 26 Nao
wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno
dogo wakaliamua wenyewe
Kwa mimi kuwa kiongozi, kazi
yangu kuu ni kuwaongoza wengine waende mbele - Kut 15:22 Musa akawaongoza Israeli waende mbele
kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya
siku tatu jangwani wasione maji (changamoto zenyewe zipo tu).
Mara ulipochaguliwa kwenye
hiyo nafasi yako, kuna mahali unapaswa uwafikishe watu unaowaongoza - Kut 32:34 Basi
sasa uende ukawaongoze watu
hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu
atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kwa ajili ya
dhambi ya
Kwa maombi umepatikana,
hata kama ulipigiwa kura ama uliteuliwa - Numbers 27: 15 Musa
akanena na Bwana akisema, 16 Bwana, Mungu wa roho za wenye mwili wote, na aweke mtu juu ya
mkutano, 17 atakayetoka mbele yao, na kuingia mbele yao; atakayewaongoza
watokapo, na kuwaleta ndani; ili mkutano wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na
mchungaji. (Umuhimu wa kiongozi unabainika hapa - usijidharau)
Pamoja na baadhi ya vigezo,
watu huchaguliwa kuwa viongozi wa wengine - 1 Nya 15: 19 Hivyo
hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba
kwa sauti kuu; 20 na Zekaria, na Yaasieli na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na
Eliabu, na Maaseya, na Benaya, wenye vinanda vya sauti ya Alamothi; 21 na
Matithiya, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, na Azazia, wenye
vinubi vya sauti ya Sheminithi, 22 waongoze. Na Kenania, mkuu wa Walawi, alikuwa juu ya uchukuzi; yeye aliusimamia uchukuzi, kwa sababu alikuwa mstadi. 23 Na
Berekia na Elkana walikuwa
mabawabu kwa ajili ya sanduku.
Kuwa na kiongozi ni mbinu
nyingine muhimu ya kusonga mbele - 1 Nya 19:16 Na Washami walipojiona
kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, wakapeleka wajumbe, wakawavuta Washami
walioko ng'ambo ya Mto, na Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza.
Njia kutonyooka wakati
wote, kiongozi lazima kujipa moyo ni muhimu sana ili kufikia malengo - 2 Nya
25:11 Amazia akapiga moyo konde, akawaongoza watu wake, akaenda mpaka Bonde la Chumvi,
akawapiga katika wana wa Seiri watu elfu kumi.
Je, kuna siku umewahi
kujitambua kuwa wewe ni kiongozi wa ngazi hiyo uliyoko? Ayu 31:18 Nami
nimekuwa ni kiongozi cha
mjane tangu tumbo la mamangu
Kiongozi anapoharibika,
waongozwao huonewa na chochote - Isa 3:12 Katika habari za watu wangu,
watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu
njia ya mapito yako. Na ikifikia hatua ya kiongozi kuwakosesha
watu wa Mungu, Mungu kuanza kulalamika - Isa 9:16 Kwa
maana wawaongozao watu
hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu
hao wameangamia.
Waongozwao nao hugundua
ubaya wa kiongozi wao - Omb 3:2 Ameniongoza na
kuniendesha katika giza Wala si katika nuru. Mungu huweka tangazo - Micah 7:5
Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini
Kiongozi kutopata maelekezo
toka kwa Mungu kupitia Neno na Maombi, hushindwa kupambanua - Mat 23:16 Ole wenu
viongozi vipofu,
ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa
dhahabu ya hekalu, amejifunga. Pia Mat 23:24 Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na
kumeza ngamia.
Kuna utofauti mkubwa sana
wa kuongoza kidunia na kuongoza kiroho - Marko 10: 42 Yesu
akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao
huwatumikisha.
43 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, 44 na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. 45 Kwa
maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake
iwe fidia ya wengi.
Tunakuwa viongozi wazuri kwa sisi wenyewe
kuongozwa kwanza na Roho Mtakatifu - John 16:13 Lakini
yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote;
kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia
atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Pia tunapewa karama za maongozi - 1Corinthians 12:28 Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili
manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na
masaidiano, na maongozi, na aina za lugha
Kiongozi mzuri huwa mfano
kwa kumheshimu kiongozi wa juu yake - Hebrews 13:7
Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza,
waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao,
iigeni imani yao. Hebrews 13:17 Watiini wenye kuwaongoza, na
kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa
hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana
isingewafaa ninyi. Hebrews 13:24 Wasalimuni wote wenye kuwaongoza, na
watakatifu wote; hao walio wa Italia wanawasalimu
Kuna faida nyingi kwa kuwa
kiongozi bora - Daniel 12:3 Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza
wa anga; na hao waongozao wengi
kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele
Ili ufanikiwe kwenye
uongozi wako, lazima ushauriane na viongozi wenzako. Usiache kuitisha vikao - 1
Nya 13:1 Kisha Daudi akafanya shauri na maakida wa maelfu, na maakida wa
mamia, naam, na kila kiongozi.
Jihoji: Kikao kikiitishwa
na huji, unakuwa umeamuaje? Kutokutafuta walau mrejesho wa kikao, ina maana
gani kwako? Unadhani udhaifu wa kiongozi wa kiroho unaambatana na ulegevu
kiroho? Kuongoza kulalamika wakati huwajibiki katika nafasi yako ni kusemaje?
Kutoshiriki semina yoyote, ina tafsiri ipi? Kama watu hawatoshi kukuelekekeza,
nani hatimaye unadhani atafaa kusema nawe? Ili ukubaliane na jambo, ni kwa njia
ipi nzuri uambiwe? Unadhani kuchaguliwa na watu kuwa kiongozi ina muunganiko
wowote na kupewa nafasi ya kuongoza na Mungu?
Kwa leo tunaishia hapa na Mungu awabariki kwa kujitambua kuwa mu
viongozi na mkakubali kuanzia sasa kuwa viongozi bora
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni