ISHI UKIJUA KUWA NI KIONGOZI
Mwl. E. Kyejo
Neno Kuu:Mdo 8:31-Akasema;Nitawezaje
kuelewa, mtu asiponiongoza?
Maandiko ya somo:
Kutoka 18:14-20,
21-23, 24-27.
Kol 3:23-25
1. UTANGULIZI:
Kazi ya Mungu kila inapotajwa
huthibitisha kuwa kuna kiongozi ambaye anawatangulia wengine. Neno la Mungu limekuwa njia ya kuonyesha
uongozi wa kweli hata katika ya jamii, ambayo watu wake hawamjui Mungu. Kiongozi siku zote huonesha njia na kusimama
katikati ya changamoto za siku kwa siku.
Changamoto katika kuwaongoza watu waliookoka ni kubwa na ngumu zaidi
kuliko kuwaongoza watu ambao hawamjui Mungu.
Kila walipo watu wawili au watatu waliokusanyika kwa jina langu mimi
nipo katikati yao.Mt 18:20. Yesu Kristo ni mwanzilishi wa uongozi.
Kiongozi ni nani?
Ni
mtu anayeongoza kikundi cha watu ili
kufikia lengo/nia walilojiwekea. Ni mtu
aliyekabidhiwa kuongoza watu ili wamjue Mungu na kuurithi uzima wa milele.
2. SIFA
ZA KIONGOZI
1 Tim 3:1-7
Biblia
inasema askofu ni mwangalizi na shemasi ni mtumishi wa kanisa.
a) Usilaumike
b) Uwe mume/mke mmoja
c) Uwe na kiasi na Busara-Kol 3 :5,2Tim 1:7
d) Uwe wa Utaratibu
e) Uwe mkaribishaji/mkarimu
f) Uwe unajua kufundisha-1 Tim 4:16
g) Usiwe mlevi
h) Si mpiga watu (mgomvi)-2 Tim2:24
i) Uwe mpole
j) Si mtu wa kujadiliana (mbishi)
k) Usiwe mtu wa kupenda fedha
l) Uweze kusimamia nyumba yako vema
·
1 Sam: 2:12
m) Uweze kutisha watoto wako katika ustahivu-adabu na
utii. Tito 1:6-9. Mf Eli.
n) Uwe unashuhudiwa mema- 1Tim 5:10;
2 kor 8:21;1 kor 5:12-13
o) Uwe unatoa sadaka zote zilizoagizwa na Mungu aliyehai
ü Mal 3:10; Mit 3:9; 1 nya 26:26
ü Mwa 7:11;Law 27:30;Hes 18:21-24
ü Kumb 12;6;14:22-29;Neh 13:12
ü Mt 23:23; Lk 18:12; Mal 3:8
3. WAJIBU
WA KIONGOZI
·
Kuwafahamu
unaowaongoza (waamini) Yn 10:2-3;Flp 2:4, 1 Kor 10:24,33
·
Unatakiwa kuwa Mlinzi
Yn10:11-12; Neh 4:9; Mdo 5:23; Flp
2:4.
·
Uwe
kielelezo-fanya kwa mfano kusema, kutenda na kuwaza. Yn 10:37-38;1 Tim 1:16
·
Uwe na Imani
(kuamini). Yn 11:40;1 The 5:8;1 Tim 1:19, 1 Tim 4 :6
·
Uwe na bidii
katika mambo yote. 2 The 3:9-10,Mfano
Eliya alionesha bidii 1 pet 5:17
·
Uwe na sikio la
Rohoni-Omba-Kol 4:2-3
·
Uwe tayari
kujifunza ili ulijue neno la Mungu. Kol 3:16
·
Dumisha
umoja/Ushirika. Yn 17:21-26;efe 4:3-4
4. MAJUKUMU
YA KIONGOZI:
a. Mzee wa
Kanisa:Hes 11:16-17; 1 Tim 5:17;Tito
1:5;Yak 5:14;Mdo 14:23
·
Kumshauri
Mchungaji kufikia maamuzi ya kulijenga
kanisa
·
Kusimamia maono
ya Mchungaji
·
Kusimamia
utendaji wa kazi ya kanisa
·
Kupokea taarifa
toka kwa mashemasi
·
Kumtia moyo
Mchungaji katika maeneo yote ya utumishi wake
·
Kuwatembelea
washirika na kuwatia moyo wanaopitia changamoto mbali mbali
·
Kumwombea
Mchungaji na familia yake.
·
Kufanya huduma ya
maombezi
b. Shemasi: 1 Tim 3:8-13.
·
Kusimamia usafi
kanisani
·
Kusimamia
taratibu zote za Ibada
·
Kupokea taarifa
za washirika walio katika maeneo yao
·
Kutoa taarifa kwa
Mzee wa kanda/mzee wa eneo
·
Kuwatembelea
washirika walio katika eneo lako
·
Kusimamia ulinzi
na usalama wa mali
za washirika kanisani
·
Kupokea washirika
na wageni katika ibada
c. Mwalimu wa
Cell: Mdo 20:20
·
Kusimamia
washirika walio katika eneo lako
·
Kuwatembelea na
kufahamu changamoto zao wanazozipitia.
·
Kuwaombea
·
Kuwafundisha
kweli yote ya neno la Mungu
·
Kusoma neno na
Kupokea mafundisho
·
Kushiriki ibada
kwa uaminifu
d. Kiongozi wa
Idara:
·
Kusimamia malengo
ya idara unayoiongoza
·
Kusimamia huduma
za idara
·
Kusimamia vikao
vya idara
·
Kutoa taarifa ya
idara yako kwa Mchungaji
·
Kusimamia maombi
katika idara
·
Kusimamia maisha
ya ushuhuda katika idara
·
Kusimamia kalenda
ya mwaka ya idara
4. HASARA ZA KIONGOZI
ASIYEKUWA TAYARI KUTUMIKA
Kiongozi akiwa hana sifa anasababisha
mkwamo wa watu au kikundi kufikia lengo ambalo walikuwa wanalitarajia.
§ Huwa na tabia za kujitenga na viongozi wenzake kwa
kila mamuzi yaliyofanyika.
§ Huwa na tabia ya kujitanguliza
§ Huwa na tabia ya kunung’unika kila wakati.Flp 2:3
§ Hukosa Uvumilivu na Upendo
§ Asiposaidiwa anaweza kusababisha maasi katika ya
kundi.
5. FAIDA
YA KIONGOZI ALIYEKUWA TAYARI KUTUMIKA:
Kiongozi mwenye sifa atasababisha kazi
ya kikundi kusonga mbele na kufikia lengo lile ambalo wamejiwekea.
o
Huwatia moyo
wengine
o
Husimamia mamuzi
ya viongozi wenzake
o
Huwatanguliza
wengine-Flp 2:4; 1 kor 10:24,33
o
Huwapenda wote
o
Huwainua watu
waliofikia kukata tamaa.
6. HITIMISHO:
v Lazima uwe tayari kumsikiliza Roho Mtakatifu
v Beba mzigo wa kuomba kila siku-1 The 5:17
v Soma Neno-Kol 3:16, 1 Pet 4:7
v Ishi Maisha matakatifu-Kol 3:5-10.
v Watangulize wengine
v Uwe mtu wa toba-Yak 5:16
Maswali na Majibu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni