Jumatano, 27 Mei 2015

Toa taarifa ya uendeshaji mbovu wa vyombo vya moto

Info Post
5/28/2015 08:33:00 AM


Kutokana na wimbi la ajali za barabarani linalosababisha vifo vya mamia ya watu na maelfu kujeruhiwa, wananchi wametakiwa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pindi wanapoona kanuni na sheria za barabarani zinakiukwa na madereva wazembe.

Namba iliyotajwa ni 0800 75 75 75 ambayo itapeleka ujumbe utakaofikishwa katika Makao Makuu ya Polisi kisha mawasiliano kufanywa na askari waliopo katika kituo kinachofuata katika barabara linakopita basi hilo ili lisimamishwe. Taarifa za kukamatwa kwa basi husika zitatangazwa moja kwa moja na Radio One na kuoneshwa ITV.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni